← Rudi kwenye Makala

MikroTik

Jinsi ya Kuseti MikroTik Hotspot Kuanzia Mwanzo hadi Mwisho

SiscoHotspot TeamMwongozo wa vitendo

Tumia mwongozo huu kama msingi wa vitendo, kisha badilisha kila hatua kulingana na mtandao, wateja na sera zako za uendeshaji.

01

Weka WAN na LAN kwanza

Seti interface ya WAN kwa IP tuli au PPPoE kutoka kwa mtoa huduma wako, kisha tengeneza interface tofauti ya LAN/bridge kwa wateja wa hotspot yenye subnet yake — usichanganye trafiki ya usimamizi na ya wateja kwenye interface moja.

02

Tengeneza hotspot server na DHCP pool

Tumia Hotspot Setup wizard (au /ip hotspot setup kwa mkono) kuunganisha hotspot server na bridge inayohudumia wateja, weka DHCP pool ya kutosha kulingana na idadi ya wateja unaotarajia kwa wakati mmoja, na weka jina la DNS watakaloliona wateja kwenye ukurasa wa kuingia.

03

Unganisha API user kabla ya kuanza kutumia

Tengeneza API user maalum mwenye password imara na ruhusa (policy) zinazohitajika na SiscoHotspot pekee (read, write, api, rest-api) — usitumie akaunti kuu ya admin — kisha jaribu muunganiko kwenye Router Management kabla ya kuuza vocha ya kwanza.

Unahitaji msaada wa kutumia haya kwenye ISP yako?

Ongea na timu ya SiscoHotspot kuhusu router, vifurushi na workflow ya malipo.

Wasiliana na Timu